2.  Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Qatar unawatangazia raia wote wa Tanzania waliokuja kwa ziara, kupita njia (on transit) na waishio nchini Qatar kuwa Ubalozi unaendelea kufanya mawasiliano ya karibu na Mamlaka za Qatar kuhusu kadhia ya suala linaloendela la mashambulizi dhidi yake na kuhakikisha usalama wa watanzania nchini Qatar kuwa ni kipaumbele cha kwanza.

3.  Aidha, pamoja na kuhakikisha usalama huo, Ubalozi unaendelea kuwasisitiza watanzania waliopo nchini Qatar kuzingatia yafuatayo:

i. Kuendelea kubaki kwenye makaazi isipokuwa penye uhitaji wa lazima wa kutoka nje;

ii. Kufuata maagizo, maelekezo, ilani, indhari na tahadhari zinazotolewa na Mamlaka za Qatar;

iii. Kuendelea kujisajili kwenye mfumo wa diaspora uliopo kwenye tovuti ya Ubalozi;

iv. Kujizuia kusambaza taarifa zisizothibitishwa na vyanzo rasmi vya habari vya Serikali na;

v. Kutunza vyema hati za kusafiria na kuweka karibu vitambulisho muhimu vya kazi na kiraia.

4.  Sanjari na taarifa hii, Ubalozi umeweka nambari za simu na barua pepe kwa ajili ya mawasiliano ya haraka na dharura kwa masaa ishirini na nne (24) kama ifuatavyo:

Simu + 974 71171700   -  Mawasiliano ya moja kwa moja
Simu + 255 764060549   -  Mawasiliano ya whatsapp

Imetolewa na:
UBALOZI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NCHINI QATAR,
DOHA, 03 MACHI, 2026