Maonesho ya Kimataifa ya Usafiri na Utalii yaliyofanyika kuanzia tarehe 16 -18 Novemba 2021 nchini Qatar. Nchi mbalimbali na makampuni ya Usafiri na Utalii yalishiriki kwenye maonesho hayo. Kwa upande wa Tanzania, Wizara ya Maliasili na Utalii (Bodi ya Utalii Tanzania), Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Mamlaka ya Viwanja vya Ndege) , Wadau wa Sekta Binafsi, Wajasiriamali na Diaspora wa Tanzania waishio nchini Qatar walishiriki kufanikisha  maonesho hayo.