Mhe. Dr. Dorothy Onesphoro Gwajima (MP), Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mhe. Riziki Pembe Juma (MHR), Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wa Zanzibar pamoja na Mhe. Habibu Awesi Mohamed, Balozi wa Tanzania nchini Qatar, wakifanya mazungumzo na Viongozi wa Kampuni ya KON Group, Mshirika wa Uwekezaji katika miradi inayohusiana na maendeleo ya jamii tarehe 31 Januari 2024.