Mhe. Habibu Awesi Mohamed, Balozi wa Tanzania nchini Qatar akikutana na Viongozi na Washiriki wa Mashindano ya “ World Aquatics Championship” yanayofanyika kuanzia tarehe 2 Februari, 2024 hadi 18 Februari, 2024. Chama cha Kuogelea Tanzania kilialikwa na “World Aquatics" kushiriki Mashindano ya Kuogelea yanayofanyika katika Ukumbi wa Aspire Dome mjini Doha. Ushiriki huwo umeongozwa na Viongozi Watatu kutoka Tanzania, Bw. David Mwasyoge - Rais wa Chama cha Kuogelea Tanzania, Bi. Inviolata Itatiro - Katibu Mkuu wa Chama cha Kuogelea Tanzania, Bi. Thauriya Diria - Mjumbe wa “Africa Aquatics Bureau” na Washiriki Wanne wa Mashindano hayo kutoka Timu ya Taifa Tanzania, Bi. Natalia Ladha, Bi. Amylia Chali, Bw. Michael Joseph na Bw. Ethan Alimanya.