Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Qatar unapenda kuwajulisha Watanzania wote waishio nchini Qatar kwamba Benki ya Biashara Tanzania (Tanzania Commercial Bank -TCB), imeanzisha utaratibu wa kutoa huduma binafsi za kibenki kwa Watanzania wanaoishi nje ya nchi kupitia “Premium and Diaspora Banking Services” ambayo ilianzishwa kwa lengo la  kutatua changamoto mbalimbali za masuala ya kibenki na kuboresha huduma zenye kukidhi mahitaji ya Watanzania waishio nje ya nchi, Wanadiplomasia walioko Ubalozini, Wafanyakazi pamoja na Wawekezaji mbalimbali.