Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeahidi kuwa  itahakikisha inatafuta fursa za ajira kwa Vijana wa Zanzibar za Serikali na zile za sekta binafsi ndani na Nje ya Zanzibar.

Akizungumza na Vijana waliofika kufanya usaili wa nafasi ya udereva Nchini Qatar huko Skuli ya Ali Hassan Mwinyi  Waziri wa Vijana Ajira na Uwezeshaji Mhe Shaaban Ali Othman amesema Serikali kupitia Wizara anayoisimamia imeaandaa  utaratibu maalum wa kuwasaidia Vijana wa kizanzibari kufikia malengo yao katika kujikwamua kiuchumi.

Amesema hatua hiyo muhimu itafikiwa kwa kuwa na mashirikiano na Taasisi mbali mbali zinazotoa ajira za mikataba au za muda mrefu pamoja na wadau wa maendeleo ya Vijana wa ndani na nje ya nchi.

Aidha amewasisitiza Vijana hao kufahamu ya kwamba hakuna Ajira zinazotolewa kwa kuuzwa na kufanya hivyo ni kosa na  yule atakaefanya hivyo atachukuliwa hatua za kisheria .

" Ajira zote ni bure ajira ni haki ya kila kijana na mimi nina wajibu kusimamia haki na maslahi ya Vijana " alisema Waziri Shaabani

Akizungumza  Katibu Mkuu Wizara ya Vijana Ajira na Uwezeshaji Salama Mbarouk Khatib ametoa wito kwa Vijana wote wa Zanzibar wenye umri kati ya miaka kumi na tano na thalathini na tano kujiunga na mabaraza ya Vijana katika Shehia zao

Aidha amefahamisha kuwa kupitia Wizara hiyo  Vijana wote ambao wana shughuli za kufanya na wanahitaji kuwezeshwa kwa lengo la kukuza  mitaji na biashara zao.

Aidha amewataka Vijana kuitumia mitandao ya kijamii kuendelea kujifunza ili kukuza taaluma zao na kupata uelewa zaidi

Nae Mkurugenzi Idara ya Ajira Zanzibar Abdalla Saleh Omar amesema kupitia Idara  hiyo itahakikisha inasimamia upatikanaji wa ajira kwa Vijana usiokuwa na urasimu kwa sekta za Serikali na binafsi.

Kwa upande wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Vijana Zanzibar Ali Haji Hassan amesema uwepo wa Mabaraza ya Vijana Zanzibar utasaidia Vijana wengi kupata fursa ikiwa ni pamoja na ajira na kuwezeshwa kwa kupewa mafunzo ya ujuzi, mitaji na vifaa.

@dr.hmwinyi @paul_christian_makonda_arusha @samia_suluhu_hassan ofisi_ya_makamu_wa_rais @owm_tz @wasafifm @millardayo @zbc_zanzibar @tbc_online @cnn @ccmtanzania @ofisi_ya_msajili_wa_hazina @ofisiyamuftimkuuzanzibar @wizara_sanaatz
                https://www.instagram.com/p/DUK-V3PCA85/?img_index=7&igsh=OWhpMXZpMjJpeTE2